Ruka hadi kwenye tangazo
Reliable industrial supply partner in Tanzania+255 69 944 2611   •   info@multflexgeneralsupply.co.tz
Transport & Logistics

Dereva wa Malori
(Truck Driver)

Ajira ya muda wote • Nyakato, Mwanza, Tanzania

Maombi yanapokelewa

Kuhusu Kampuni na Nafasi ya Kazi

Multflex General Supplies Limited ni kampuni ya Kitanzania yenye makao yake Nyakato, Mwanza, inayojihusisha na usambazaji wa vifaa vya viwandani, migodini, ujenzi, vipuri vya magari na bidhaa mbalimbali kwa wateja wake.

Kampuni inatangaza nafasi ya kazi ya Dereva wa Malori (Truck Driver) Mwanza kwa ajili ya kuimarisha shughuli zake za usafirishaji na usambazaji wa mizigo. Hii ni ajira ya muda wote (Full-Time) katika idara ya Usafirishaji na Usambazaji (Transport & Logistics).

Tunakaribisha maombi kutoka kwa madereva wenye uzoefu, weledi, nidhamu, uadilifu na uwezo wa kuendesha magari makubwa kwa kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani.

Majukumu ya Kazi

  1. Kuendesha malori kwa usalama katika safari za usafirishaji wa mizigo kulingana na maelekezo ya kampuni.
  2. Kufanya ukaguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kuhakikisha lipo katika hali nzuri ya kiufundi.
  3. Kuhakikisha mizigo inapakiwa, inalindwa na kufikishwa salama katika maeneo yaliyopangwa.
  4. Kuzingatia sheria za usalama barabarani na taratibu za usafirishaji.
  5. Kutambua hitilafu za kiufundi na kutoa taarifa kwa uongozi kwa wakati.
  6. Kutunza gari, vifaa vyake na nyaraka zote zinazohusiana na safari.
  7. Kutunza kumbukumbu za safari, matumizi ya mafuta na taarifa nyingine za uendeshaji.
  8. Kushirikiana na idara ya usafirishaji kuhakikisha huduma zinatolewa kwa wakati na kwa ufanisi.

Sifa za Mwombaji

  1. Awe na umri wa miaka 25 au zaidi.
  2. Awe na ujuzi wa ufundi wa magari na Cheti cha Ufundi Daraja A (Mechanics Certificate).
  3. Awe na leseni halali ya udereva yenye madaraja C na E.
  4. Awe na Cheti cha Defensive Driving kinachotambulika.
  5. Awe na uwezo wa kuendesha malori makubwa na kufuata taratibu za usalama.
  6. Cheti cha kuendesha magari maalum kitakuwa faida ya ziada.
  7. Cheti kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT – National Institute of Transport) kitahesabika kama faida ya ziada.
  8. Awe mwaminifu, mwenye nidhamu, anayewajibika na anayeweza kufanya kazi kwa ushirikiano.

Nyaraka za Kuambatanisha

  • Barua ya maombi ya kazi.
  • Wasifu binafsi (CV) ulioboreshwa.
  • Nakala ya leseni halali ya udereva.
  • Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
  • Cheti cha LATRA.
  • Nakala za vyeti husika vya taaluma na udereva.
  • Taarifa ya eneo analoishi mwombaji kwa sasa (Current Location).

Jinsi ya Kutuma Maombi

Waombaji wote wenye sifa wanakaribishwa kutuma maombi na nyaraka zao kupitia barua pepe: hr@multflexgeneralsupply.co.tz.

Mada ya barua pepe (Email Subject):
Maombi ya Kazi – Dereva (Truck Driver)

Barua ielekezwe kwa:

Human Resource Manager
Multflex General Supplies Limited
Nyakato, Mwanza, Tanzania.

Hakikisha nyaraka zote muhimu zimeambatanishwa kabla ya kutuma maombi. Bonyeza kitufe hapa chini kufungua programu yako ya email, kisha ambatanisha nyaraka na utume.

Tuma Maombi kwa Email →

Tarehe ya mwisho ya maombi: Haijatangazwa.

Kumbuka: Waombaji watakaokidhi vigezo vya awali pekee ndio watakaowasiliana nao kwa hatua zinazofuata za usaili.

Fahamu zaidi kuhusu Multflex General Supplies Limited na huduma zetu za usafirishaji na usambazaji.